Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

يَمْحَقُ اللَّـهُ الرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ

”Allaah huifuta baraka [mali ya mali ya] ribaa na huzibariki swadaqah; na Allaah hampendi kila aliye mwingi wa kukufuru, mwenye madhambi.”[1]

Umesema kweli, ee Mola wetu! Hakika tumeona benki nyingi zinazofanya biashara za ribaa jinsi zinavyoanguka na kufilisika. Tumeona jinsi familia nyingi zinazojishughulisha na ribaa wameziacha familia zao wakawa ni masikini. Kwa hivyo Aayah ni yenye kuenea na inahusu ribaa kubwa na ribaa ndogo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amemlaani mla ribaa, mwenye kuitoa, mwenye kuiandika na mashahidi wake.”[2]

Ukijua kuwa wanajenga nyumba inayotokana na ribaa au benki ya ribaa, basi haijuzu kwako kufanya kazi mahali hapo. Wala haijuzu hata kufanya kazi ya mtengeneza sakafu au mlinzi wa nyumba katika sehemu kama hizo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwili wowote uliokulia juu ya haramu, basi Moto una haki nao zaidi.”[3]

Hii leo kuna fatwa za kipotofu zinazotoka kwa Muhammad al-Ghazaaliy zinazosema kuwa ni sawa kufanya kazi katika benki za ribaa na serikali. Kisha anasema kuwa hakuna anayepinga jambo hilo isipokuwa tu watu wenye msimamo mkali. Baadhi ya wajinga na watu waliopinda wanamwita Muhammad al-Ghazaaliy huyu kuwa ni “mlinganizi mkubwa”. Ni kweli kwamba ni mlinganizi mkubwa, lakini katika upotofu.

[1] 2:276

[2] Muslim.

[3] at-Tirmidhiy (610). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh at-Tirmidhiy” (1/336).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 278
  • Imechapishwa: 16/04/2025