Swali: Je, ni lazima mbinu za kulingania ziwe kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah au ni kutokana na Ijtihaad ya mtu mwenyewe?

Jibu: Haijalishi kitu, hatutakiwi kwenda kunyume na dalili kwa maoni yetu. Inafaa kwa mlinganizi kulingania muda wa kuwa haendi kinyume na Qur-aan na Sunnah. Anaweza kulingania wakati wowote anaotaka kwa sharti asiendi kinyume na Qur-aan na Sunnah. Ulingano ambao unaenda kinyume na Qur-aan na Sunnah Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) haubariki. Allaah (´Azza wa Jall) amemwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

ادْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِالْحِكْمَةِ وَالْمَوْعِظَةِ الْحَسَنَةِ ۖ وَجَادِلْهُم بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Lingania katika njia ya Mola wako kwa hekima na mawaidha mazuri na jadiliana nao kwa ambayo ni mazuri zaidi.”[1]

Ikiwa hekima ni kunyamaza, basi anyamaze, na ikiwa ni kuzungumza, basi azungumze:

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي

“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi – mimi na anayenifuata.”[2]

Lakini asiingize ndani ya ulinganizi yasiyokuwemo, kama mfano wa maigizo na mfano wake. Baadhi ya walinganizi wasiokuwa na elimu ya Qur-aan na Sunnah wanasema kuwa mtu asiwazungumzishe watu kwa Aayah za Qur-aan na Hadiyth za kinabii; wazungumzishe kutoka kichwani mwako. Hilo ni kwa sababu amekosa elimu ya Qur-aan na Sunnah.

[1] 16:125

[2] 12:108

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 396-397
  • Imechapishwa: 23/06/2025