Mlezi wa mayatima kujipa zakaah kutoka katika mali yao

Swali: Nina deni kubwa linalokaribia 200.000 nami ni mlezi wa ndugu yangu mdogo ambaye ana mali ninayotoa zakaah yake. Je, inajuzu kwangu kuchukua kutoka katika zakaah hiyo?

Jibu: Mlezi hachukui zakaah, bali huwapa mafakiri na wala hachukui kwa ajili ya nafsi yake; kwa kuwa yeye ni mwenye jukumu na anatuhumiwa. Hivyo mlezi wa mayatima hutoa zakaah yao kwa wengine, si kujipa mwenyewe.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30091/هل-يجوز-للوكيل-المحتاج-الاخذ-من-زكاة-موكله
  • Imechapishwa: 07/09/2025