Swali: Wanazuoni wakaguzi wanasemaje kuhusiana na Hadiyth inayosema:

”Mkosi uko katika vitu vitatu.”?

Je, kuna mgongano na yale yaliyopokelewa kwamba aliwaambia watu wa familia yake:

”Acheni, kwa hakika ni kitu kibaya.”?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mkosi uko katika vitu vitatu; kwenye mnyama wa kipando, kwenye mwanamke na kwenye nyumba.”

Inawezekana kuwepo mkosi katika nyumba, kwa mwanamke au kwa mnyama. Akiuona kuwa nyumba haimfai, mnyama hamfai au mwanamke hamfai, basi hakuna ubaya kuitoka nyumba hiyo, kumuacha mnyama huyo au kumpa mwanamke huyo talaka. Hili hutambulika kutokana na hali ya mnyama, hali ya nyumba au hali ya mwanamke. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kwa kukata kauli:

”Mkosi uko katika vitu vitatu.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31705/ما-معنى-حديث-ان-كان-الشوم-ففي-ثلاثة
  • Imechapishwa: 03/12/2025