Swali: Kuna mwanaume ameoa lakini mkewe hamtoshelezi. Kila anapoona mwanamke mwingine ni kama vile hajaoa kwa sababu ambazo Allaah anazijua. Mkewe amemwambia akioa basi amwache. Je, aowe mke wa pili bila ya kumjulisha kisha baadaye amwambie, hali ya kuwa mke huyu ni mwenye hasira sana au akimzuia ndio amtaliki? Je, kuoa wake wa pili kunakuwa ni wajibu kwake kwa sababu mke wa kwanza hamtoshelezi?
Jibu: Iwapo hamtoshelezi basi inamlazimu aowe mke mwingine ikiwa anaweza, aowe mke wa pili. Iwapo wa pili naye hamtoshelezi, aowe wa tatu. Iwapo wa tatu naye hamtoshelezi, aowe wa nne ili ajitosheleze nafsi yake ikiwa ana uwezo na ana mali, japo mke wake hataridhia. Lakini awaridhishe wote kwa maneno mazuri, kwa mbinu njema na kwa uadilifu. Ni juu yake kujitahidi kuwa mwenye uadilifu na kumuomba Mola wake awaongoze na awajaalie ridhaa. Ajitahidi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً
“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne.”[1]
Haijuzu kwa mwanamke kumpinga katika jambo hili. Ikiwa hawezi kuvumilia, kwa maana ya kwamba ni mwenye dhiki, uzito na kushindwa, basi ampe ruhusa ufumbuzi.
[1] 04:03
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30079/هل-يجب-التعدد-على-من-لا-تعفه-زوجته
- Imechapishwa: 06/09/2025
Swali: Kuna mwanaume ameoa lakini mkewe hamtoshelezi. Kila anapoona mwanamke mwingine ni kama vile hajaoa kwa sababu ambazo Allaah anazijua. Mkewe amemwambia akioa basi amwache. Je, aowe mke wa pili bila ya kumjulisha kisha baadaye amwambie, hali ya kuwa mke huyu ni mwenye hasira sana au akimzuia ndio amtaliki? Je, kuoa wake wa pili kunakuwa ni wajibu kwake kwa sababu mke wa kwanza hamtoshelezi?
Jibu: Iwapo hamtoshelezi basi inamlazimu aowe mke mwingine ikiwa anaweza, aowe mke wa pili. Iwapo wa pili naye hamtoshelezi, aowe wa tatu. Iwapo wa tatu naye hamtoshelezi, aowe wa nne ili ajitosheleze nafsi yake ikiwa ana uwezo na ana mali, japo mke wake hataridhia. Lakini awaridhishe wote kwa maneno mazuri, kwa mbinu njema na kwa uadilifu. Ni juu yake kujitahidi kuwa mwenye uadilifu na kumuomba Mola wake awaongoze na awajaalie ridhaa. Ajitahidi. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:
فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً
“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne.”[1]
Haijuzu kwa mwanamke kumpinga katika jambo hili. Ikiwa hawezi kuvumilia, kwa maana ya kwamba ni mwenye dhiki, uzito na kushindwa, basi ampe ruhusa ufumbuzi.
[1] 04:03
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30079/هل-يجب-التعدد-على-من-لا-تعفه-زوجته
Imechapishwa: 06/09/2025
https://firqatunnajia.com/mke-wa-kwanza-hamtoshelezi/