Mke wa Isak anajisitiri katika Biblia

61Kisha Rebeka na wajakazi wake wakapanda ngamia na kumfuata huyo mtumishi wa Abrahamu; nao wote wakaondoka.

62Wakati huo, Isaka alikuwa ameondoka Beer-lahai-roi, akawa anakaa huko pande za Negebu. 63Siku moja jioni, Isaka alikwenda mashambani kutafakari. Basi, akatazama akaona ngamia wanakuja. 64Naye Rebeka alipotazama na kumwona Isaka, alishuka chini 65na kumwuliza mtumishi wa Abrahamu: “Ni nani yule mtu anayetembea kule shambani, anakuja kutulaki?” Yule mtumishi akasema: “Ni bwana wangu.” Basi, Rebeka akachukua kitambaa cha kichwani akajifunika.

66Yule mtumishi akamsimulia Isaka yote aliyokuwa ameyafanya. 67Basi, Isaka akamchukua Rebeka ndani ya hema iliyokuwa ya Sara mama yake, akawa mke wake. Isaka akampenda Rebeka na kupata faraja baada ya kifo cha mama yake.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mwanzo 24:61-66
  • Imechapishwa: 15/01/2020