Mke alifanya ghushi kurudisha bikira ya bandia

Swali: Mwanamke ameolewa na hakuwa bikira. Akafanyiwa hatua za kurudisha bikira ili mambo yasionekane. Kisha akazaa watoto wawili. Baada ya hapo akasikia fatwa ya kwamba ndoa hii ni batili. Na pindi alipomuuliza Shaykh wa karibu nae akamwambia ajisitiri. Ni ipi nasaha yako kwangu Shaykh na je ametalikika kwa kuwa hawezi kumuwekea wazi mume wake?

Jibu: Ndoa ni sahihi – Allaah akitaka. Lakini hata hivyo ulifanya ghushi. Ni lazima kwako kufanya tawbah na kuomba msahama. Maadamu ndoa yako ni sahihi, watoto wako kwa mwanaume huyo ni watoto wa Kishari´ah. Na Allaah anajua zaidi.

Check Also

Mke anachukua pesa kutoka kwa mume kwa ajili ya haja za mustakabali

Swali: Mke anachukua pesa kutoka kwa mume wake na anasema kuwa ni kwa ajili ya …