Mkazi wa Qasiym ameingilia Ihraam Twaaif

Swali: Kuna mtu alisafiri kutokea Qasiym kwa ajili ya kutaka kufanya ´Umrah. Lakini njiani akasimama Madiynah kwa muda wa siku tatu na baadaye akaendelea Jeddah ambapo na huko akakaa kwa muda wa siku tatu. Kisha akaenda Twaaif na akaingia Ihraam kutokea hapo Twaaif.

Jibu: Analazimika kutoa fidia. ´Umrah yake ni sahihi lakini atalazimika kutoa fidia, kwa sababu ameingia Ihraam kutoka kwenye kituo alichokipita, nacho ni Dhul-Hulayfah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (20) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-6-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 10/01/2020