Swali: Siku nyingine zisizo ya ijumaa, ikiwa mkataba wa biashara umefanyika baada ya kukimiwa kwa swalah?

Jibu: Si halali kwake kuchelewa na swalah kwa ajili ya biashara. Inampasa aharakie kwenda kuswali pamoja na mkusanyiko. Si halali kwake kuchelewa.

Swali: Je, mkataba wa biashara huo ni sahihi?

Jibu: Sijui kizuizi chochote, kwa kuwa Maandiko yapo maalum kwa mwito wa ijumaa. Lakini si halali kwake kuchelewa wala kufanya biashara inayomzuia na swalah ya faradhi. Inampasa aharakie katika swalah ya faradhi – ni mamoja iwe Dhuhr, ´Aswr, Maghrib au ´Ishaa – hata kama si ijumaa, kwani hilo ni jambo la wajibu kwake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31564/ما-حكم-البيع-بعد-اقامة-الصلاة-يوم-الجمعة
  • Imechapishwa: 02/11/2025