al-Hajuuriy ana misingi iliyopinda anayofuata yeye na wafuasi wake. Misingi hii inamtoa katika mfumo wa wanachuoni. Hii hapa inayofuata ni baadhi ya misingi aliyokhalifu Yahyaa al-Hajuuriy:

Msingi wa kwanza: Umoja.

Msingi wa pili: Kuwapenda Ahl-us-Sunnah wote.

Msingi wa tatu: Kulinda nafasi za wanachuoni.

Msingi wa nne: Kuwasifu maimamu waliotangulia.

Msingi wa tano: Hekima wakati wa kulingania katika dini ya Allaah.

Msingi wa sita: Kuwaachia wanachuoni ndio wahukumu wakati wa fitina na majanga yanayotokea.

Msingi wa saba: Kuwa na msimamo juu ya Sunnah na usalama kutokamana na wingi wa kupinda.

Hii ni msingi saba na huenda kukaja mingine huko mbeleni.

Ilipokuwa kwenda kinyume na misingi hii ndio sababu ya yeye na wafuasi wake kupinda ndipo nikapendelea kuibainisha ili mpenzi msomaji aweze kutambua ni kwa sababu gani wanachuoni wamemtahadharisha al-Hajuuriy na wafuasi wake.

Kila mwenye busara na mwadilifu anatambua ya kwamba kitendo cha wanachuoni kumtahadharisha al-Hajuuriy, Falaah al-Harbiy na wafuasi wao ni dalili tosha inayoonyesha kuwa Ahl-us-Sunnah ni watu wenye inswafu wasiompaka mafuta yeyote inapokuja katika dini ya Allaah (Ta´ala). Haijalishi kitu hata kama mtu huyo mwanzoni alikuwa akijinasibisha nao. Hata kama mtu atakuwa ni mwenye kujifanya kuwaraddi Ahl-ul-Bid´ah na watu wa vikundivikundi hawawi radhi naye mpaka anyooke juu ya njia ya sawa.

  • Mhusika: Shaykh Abu ´Ammaar ´Aliy al-Hudhayfiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://m-noor.com/showthread.php?p=33728
  • Imechapishwa: 14/01/2017