Misikiti inayojengwa na wasanii

Swali: Kipindi cha mwisho ni jambo linatokea mara nyingi wasanii kujenga misikiti. Ni ipi hukumu ya hilo? Kama ni kitendo cha haramu ni kwa nini basi hakikatazwi?

Jibu: Kujenga msikiti ni kitu sahihi. Lakini anatakiwa kutumia juu yake chumo zuri. Jengo likikamilika kutokana na matumizi ya haramu yaliyotokamana na muziki, benki au mfano wake inasihi na kutaswaliwa ndani yake na haidhuru. Dhambi zinamrudilia yule aliyechuma haramu.

Kuhusu msikiti wenyewe ni jambo la kheri. Vivyo hivyo inahusiana na mambo mengine ya kheri inafaa kutumia juu yake pesa iliyopotea, pesa iliyochumwa kutoka katika njia isiyokuwa nzuri. Kwa sababu ni kama pesa iliyopotea na mali ambayo haina mmiliki wa kihakika. Pesa kama hii inatumiwa katika kutengeneza barabara, kutengeneza vyoo, kuwapa swadaqah mafukara, kulipa madeni ya wenye madeni, kuwasaidia wahitaji na kuwawezesha kuoa wenye kuhitajia kuoa. Kwa sababu hiyo ni kama pesa yenye utata na iliyopotea. Haina mmiliki wa kihakika.

Vivyo hivyo inahusiana na pesa ya malaya, kipato cha kuhani na pia kile kinachotokamana na ribaa na Allaah akampa nacho mwenye nacho, vitu kama hivi inafaa kutolewa katika njia za kheri. Hata hivyo inatakiwa kuitakasa misikiti kutokamana na vitu hivi na kusitumiwe juu yake isipokuwa matumizi mazuri.  Lakini pale kutapojengwa kutokamana na chumo lisilokuwa zuri, itasihi kuswali ndani yake na wala hautobomolewa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/ما-حكم-بناء-المساجد-من-كسب-حرام
  • Imechapishwa: 07/06/2020