Swali: Unasemaje juu ya mtu anayesema kuwa eti yeye anaichukua elimu yake tu kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah na wala haichukui kutoka kwa wanazuoni kwa kutumia hoja kuwa eti Mtume ametukamilishia dini.
Jibu: Mtume ameamrisha kuchukua elimu kutoka kwa wanazuoni. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesem:
فَاسْأَلُواْ أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ
“Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyoye mwenye kuchukua njia akifuta elimu katika njia hiyo, basi Allaah atamsahilishia njia ya kuelekea Peponi.”[2]
Hakusema mtu akae nyumbani kwake na akasoma vitabu. Ni lazima ashike njia ima kwa kusafiri, kwa kuketi kwa wanazuoni na mizunguko ya kielimu. Hizi ndio njia za kusoma na za njia za elimu. Sio katika njia za elimu ukachukua kitabu na kusoma na ukajidai kuwa kitabu hicho kinakutosha, unakifahamu na kadhalika. Hilo ni kosa. Hizo sio katika njia za kutafuta elimu. Njia hiyo wewe ndiye umeizua, sio katika njia za kutafuta elimu. Kitabu unakisoma kwa wanazuoni, wanakupambanulia, wanakubainishia yaliyomo ndani yake ya sahihi na yasiyokuwa sahihi.
[1] 16:43
[2] Muslim (38) na (2699).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
- Imechapishwa: 18/02/2024
Swali: Unasemaje juu ya mtu anayesema kuwa eti yeye anaichukua elimu yake tu kutoka ndani ya Qur-aan na Sunnah na wala haichukui kutoka kwa wanazuoni kwa kutumia hoja kuwa eti Mtume ametukamilishia dini.
Jibu: Mtume ameamrisha kuchukua elimu kutoka kwa wanazuoni. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesem:
فَاسْأَلُواْ أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لاَ تَعْلَمُونَ
“Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui.”[1]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yeyoye mwenye kuchukua njia akifuta elimu katika njia hiyo, basi Allaah atamsahilishia njia ya kuelekea Peponi.”[2]
Hakusema mtu akae nyumbani kwake na akasoma vitabu. Ni lazima ashike njia ima kwa kusafiri, kwa kuketi kwa wanazuoni na mizunguko ya kielimu. Hizi ndio njia za kusoma na za njia za elimu. Sio katika njia za elimu ukachukua kitabu na kusoma na ukajidai kuwa kitabu hicho kinakutosha, unakifahamu na kadhalika. Hilo ni kosa. Hizo sio katika njia za kutafuta elimu. Njia hiyo wewe ndiye umeizua, sio katika njia za kutafuta elimu. Kitabu unakisoma kwa wanazuoni, wanakupambanulia, wanakubainishia yaliyomo ndani yake ya sahihi na yasiyokuwa sahihi.
[1] 16:43
[2] Muslim (38) na (2699).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ta´liyqaat ´alaa Risaalah wujuub-il-´Amr bil-Ma´ruuf wan-Nahiy ´an al-Munkar (05)
Imechapishwa: 18/02/2024
https://firqatunnajia.com/mimi-nitasoma-qur-aan-na-sunnah-peke-yangu-na-siwahitaji-wanazuoni/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)