Swali: Je, mlango wa shaytwaan wa tatu uliotajwa unayo dalili ndani ya Qur-aan?

Jibu: Ndio, una dalili katika Qur-aan. Ukitafakari kuhusu ghadhabu, ni jambo linalojulikana kuwa ni miongoni mwa sababu za shaytwaan. Muusa alipochukia akazirusha mbao ambazo zilikuwa na maneno ya Mola wake (´Azza wa Jall).

Kuhusu ghafla Allaah amesema juu yake:

وَلَقَدْ ذَرَأْنَا لِجَهَنَّمَ كَثِيرًا مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ ۖ لَهُمْ قُلُوبٌ لَّا يَفْقَهُونَ بِهَا وَلَهُمْ أَعْيُنٌ لَّا يُبْصِرُونَ بِهَا وَلَهُمْ آذَانٌ لَّا يَسْمَعُونَ بِهَا ۚ أُولَـٰئِكَ كَالْأَنْعَامِ بَلْ هُمْ أَضَلُّ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الْغَافِلُونَ

“Hakika Tumeumba Moto wa Jahannam kwa ajili ya wengi katika majini na watu – wana nyoyo, lakini hawafahamu kwazo na wana macho, lakini hawaoni kwayo na wana masikio, lakini hawasikii kwayo – hao ni kama wanyama, bali wao ni wapotovu zaidi. Hao ndio walioghafilika.”[1]

Vilevile amesema:

وَمَن يَعْشُ عَن ذِكْرِ الرَّحْمَـٰنِ نُقَيِّضْ لَهُ شَيْطَانًا فَهُوَ لَهُ قَرِينٌ

”Anayejifanya kipofu na ukumbusho wa Mwingi wa rehema, basi Tunamwekea shaytwaan awe ndiye rafiki yake mwandani.”[2]

Kwa maana ni mwenye kughafilika.

Kuhusu shahawa dalili zake ni nyingi. Allaah amesema:

إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَمَا تَهْوَى الْأَنفُسُ

”Hawafuati isipokuwa dhana na yale yanayotamani nafsi zao.”[3]

وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللَّـهِ

”Na nani mpotofu zaidi kuliko yule aliyefuata matamanio yake pasi na uongofu kutoka kwa Allaah?”[4]

وَأَمَّا مَنْ خَافَ مَقَامَ رَبِّهِ وَنَهَى النَّفْسَ عَنِ الْهَوَىٰ فَإِنَّ الْجَنَّةَ هِيَ الْمَأْوَىٰ

“Ama yule aliyekhofu kisimamo mbele ya Mola wake na akaikataza nafsi yake na matamanio, basi hakika mabustani ndio makaazi yake.”[5]

[1] 07:179

[2] 43:36

[3] 53:23

[4]28:50

[5] 79:40-41

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31126/ما-مداخل-الشيطان-الثلاثة-وما-ادلتها
  • Imechapishwa: 05/10/2025