Mikutano na daura zinazoandaliwa na al-Ikhwaan al-Muslimuun na Jamaa´at-ut-Tabliygh

Swali: Niende katika mkutano au daura ambazo waandaaji ni al-Ikhwaan al-Muslimuun au Jamaa´at-ut-Tabliygh?

Jibu: Makundi haya yaliyotajwa yanajulikana kwa Da´wah za harakati zinazoenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.

al-Ikhwaan al-Muslimuun ni kundi ambalo linachotaka ni kukusanya vijana kama maaskari. Wanataka kuwaandaa kwa ajili ya Jihaad ya umoja ili waweze kurejesha ukhalifah ambao wanapigania.

Kuhusiana na Jamaa´at-ut-Tabliygh wengi ni wajinga kwa sababu tu wanataka kupigana na viumbe. Kuna matunda yepi mazuri kwa mtu ambaye ni mjinga au mtu ambaye anajua wanayoamini lakini bado akawa anaenda nao na kukubali Bid´ah zao na makosa yao ya wazi?

Kutokana na sababu hii na nyinginezo haipaswi kuongeza idadi yao. Elimu haipaswi kuchukuliwa kwao maadamu kuna mwanachuoni wa ki-Salafiy anayefuata Qur-aan na Sunnah. Dunia haotokuwa kamwe tupu kwa watu kama hawa.

Watu hawa wanatakiwa kutunzwa kwa mawaidha, ukumbusho na kwa dalili sahihi na ulinganio wa haki na kweli. Yule mwenye kuchukua mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na akaachana na makosa yake ya hapo mwanzo amefanya wajibu wake. Mwenye kukataa kupokea amefikiwa na haki. Mtu huyu hakuna lakumfanya. Badala yake inatakiwa kutahadharisha naye na mfumo wake.

  • Mhusika: ´Allâmah Zayd bin Muhammad bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuzhat-ut-Qaariy, uk. 176-177
  • Imechapishwa: 22/04/2015