Migahawa inatakiwa kufungwa mchana wa Ramadhaan

Swali:  Kaka yangu anamiliki mgahawa katika nchi ya kikafiri. Anauliza kama inafaa kwake kufungua mgahawa mchana wa Ramadhaan au hapana. Ndani ya nchi kuna waislamu.

Jibu: Hapana, asifungue mchana wa Ramadhaan. Ni muonekano wenye kwenda kinyume na mfumo wa Uislamu. Haifai kula wala kunywa mchana. Aheshimu mwezi na wala asifungue hata kama atakuwa katika nchi ya kikafiri. Yeye ni muislamu na anauwakilisha Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-qrran-19-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020