Mfano wa upumbavu wa Raafidhwah

Katika upumbavu wao ni kwamba wanawafananisha wale watu wanaowachukia kuwa kama viumbe visivyokuwa na uhai au wanyama. Halafu wanayafanya mambo juu ya viumbe hivyo visivyokuwa na uhai na wanyama ambayo wanayachukulia kuwa ni adhabu kwa wale watu wanaowachukia. Kwa mfano wanamchukua kondoo mwekundu na kumwita “´Aaishah”. Baada ya hapo wanamuadhibu vibaya sana na kujaalia kwamba huko ni kumuadhibu ´Aaishah.

Mfano mwingine ni kwamba wanachukua kitako cha pamba na wanajaza ndani yake mafuta. Baada ya hapo wanakipasua na yale mafuta yanakuwa yanatiririka na huku wanayanywa. Wanasema kwamba kufanya hivi ni kama mfano wa kumpasua ´Umar na kunywa damu yake.

Mfano mwingine ni kwamba utawaona baadhi yao namna wanavyowapa majina punda wao wa starehe “Abu Bakr” na “´Umar”. Kisha baada ya hapo wanawaadhibu na wanaona kwamba uhakika wa mambo wamemuadhibu Abu Bakr na ´Umar.

Wakati mwingine huandika majina yao kwenye nyayo zao na imetokea kwamba baadhi ta watawala wamewapiga nyayo zao na wakasema:

“Hakuna mwingine niliyempiga isipokuwa Abu Bakr na ´Umar na nitaendelea kuwapiga mpaka watokomee.”

Wako wengine ambao wamewapa majina mbwa wao “Abu Bakr” na “´Umar” na wakawalaani. Mmoja akimwita mbwa wa mwenzake “Bukayr”, basi anachukulia vibaya na kusema:

“Unamwita mbwa wangu jina la watu wa Motoni.”

Wengine wanamuadhimisha mwabudumoto Abu Lu´lu-ah ambaye alikuwa mtumwa wa al-Mughiyrah bin Shu´bah ambaye ndiye aliyemuua ´Umar. Wanamuadhimisha mtu, mtu kuna maafikiano juu ya ukafiri wake, kwa sababu tu alimuua ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh).

Katika upumbavu wao ni kwamba wanazua makaburi. Mara nyingi wamewadanganya watu na kuwaambia kwamba huyo aliyezikwa hapo ni mtu kutoka katika familia ya Mtume (Swalla Alalahu ´alayhi wa sallam). Wakati mwingine huenda ikawa ni mtu aliyekufa hapo na wakajenga juu yake kaburi. Pengine hata ikawa ni kaburi la kafiri au mtu mwingine.

Kuwatesa wanyama kwa njia kama hii ni jambo ambalo halifanywi na watu wengine isipokuwa tu wapumbavu na wajinga. Tungelitaka kumuadhibu Fir´awn, Abu Lahab na Abu Jahl na makafiri wengine ambao kuna maafikiano juu ya ukafiri wao kwa kutumia njia kama hii, basi ingelikuwa ni ujinga mkubwa. Kwa sababu ni jambo lisilokuwa na faida yoyote.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (1/49-50)
  • Imechapishwa: 15/12/2018