Mfano wa Tawassul ya shirki na ya kizushi

Swali: Kuna maeneo Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) katika ”at-Tawassul wal-Wasiylah” amesema kuwa Tawassul ni Bid´ah, maeneo mengine akasema kuwa ni njia inayopelekea katika shirki na maeneo mengine akasema kuwa kwamba ni shirki. Je, matamshi yote haya ni kutoka kwake?

Jibu: Mimi nimeshakuwekeeni jambo hili wazi. Tawassul ikiwa imeambatana na kumwabudu yule unayemfanyia Tawassul kama vile kumchinjia, kumuwekea nadhiri na kumwomba msaada, hiyo ni Tawassul ya shirki. Lakini Tawassul ambayo haikuambatana na kumwabudu yule unayemfanyia Tawassul, ni Bid´ah na njia inayopelekea katika shirki.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Durr an-Nadhwiyd (01)
  • Imechapishwa: 07/03/2025