Mfano wa mambo ambayo kila mtu anaweza kulingania


Swali: Mimi napenda kulingania katika dini ya Allaah na ni mwenye hamasa. Hata hivyo sina mtindo mzuri. Je, inatosha kwangu kuchagua kaseti ya mmoja katika wanachuoni na walinganizi na kuwapa zawadi ndugu na waislamu wote kwa ujumla?

Jibu: Ndio, kaseti ikiwa ni ya mwanachuoni anayetambulika kwa ´Aqiydah nzuri na elimu kubwa ukiwapa ndugu zako basi umefanya jambo zuri na unapata mfano wa thawabu wanazopata wao. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule mwenye kuelekeza katika kheri basi anapata mfano wa ujira wake.”

Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.

Kuhusu wewe hakuna kikwazo kuzungumza kwa yale unayoyajua katika haki kwa njia nzuri. Kwa mfano unaweza kuwasisitiza watu juu ya swalah ya mkusanyiko, kutoa zakaah na kuwatahadharisha usengenyi, uvumi, kuwaasi wazazi, kukata udugu na madhambi mengine aliyoyaharamisha Allaah. Kwani mambo kama haya na mfano wake ni yenye kutambulika kwa wanachuoni na waislamu wengine wa kawaida.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/69)
  • Imechapishwa: 20/02/2021