Mfano wa madhambi yenye kudharauliwa

Swali: Nini maana ya:

”… madhambi yenye kudharauliwa.”?

Jibu: Ni yale madhambi ambayo mtu anayadharau. Ni madhambi anayoyaona kuwa ni madogo na hivyo anakuwa na ujasiri wa kuyafanya. Mfano wa kuiba pesa kidogo ambacho hazimfanyi kukatwa mkono, kumgusa mwanamke, kuwatazama baadhi ya wanawake wasiokuwa na Mahaarim zao na kadhalika. Ni yale madhambi yasiyokuwa na makemeo, ghadhabu, laana, Moto wala adhabu ulimwenguni. Kikosi kikubwa cha wanazuoni wanaona kuwa mfano wa madhambi kama hayo ndio madogo na yenye kudharauliwa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24351/ما-معنى-محقرات-الذنوب
  • Imechapishwa: 02/10/2024