Swali: Ni wajibu kwa mtu aliye na meno ya bandia kuyaondosha wakati wa kusukutua?
Jibu: Mtu akiwa na meno ya kubandika lililo dhahiri ni kwamba sio wajibu kwake kuyaondosha. Hili limeshabihiana na pete. Sio wajibu kuvu pete wakati wa kutawadha. Bali lililo bora ni yeye kuitikisa. Lakini hata hivyo sio kwa njia ya uwajibu. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akivaa pete. Haikupokelewa ya kwamba alikuwa akiivua wakati wa kutawadha. Ni jambo liko wazi katika kutozuia maji kufika katika meno haya na khaswa khaswa ukizingatia ya kwamba baadhi ya watu inakuwa vigumu kuyaondosha meno haya ya bandia na baadaye kuyarudisha.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/140)
- Imechapishwa: 30/06/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)