Baadhi ya fadhila za kudumu na wudhuu´

Swali: Ni fadhila zipi anazopata muislamu akiwa na mazowea ya kutawadha kila unapomchenguka?

Jibu: Fadhila anazopata muislamu anaposhika wudhuu´ kila unapomchenguka ni kuwa anabaki hali ya kuwa na twahara. Kubaki na wudhuu´ ni miongoni mwa matendo mema. Jengine ni kwamba huenda akamdhuru Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) katika hali yote hiyo. Anakuwa amemdhukuru Allaah akiwa na twahara. Jengine vilevile ni kwamba huenda swalah ikamfikia akiwa sehemu ambayo hakuna maji. Mtu kama huyu anakuwa yutayari kwa ajili ya swalah hii. Muhimu ni kwamba mtu kubaki na wudhuu´ ndani yake kuna faida nyingi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/140)
  • Imechapishwa: 30/06/2017