Swali: Hadiyth:

”Hauondoi uchawi isipokuwa mchawi.”?

Jibu: Haya ni maneno ya baadhi ya Salaf, maneno ya al-Hasan (Rahimahu Allaah). Maana yake ni sahihi. Maana ya kwamba uchawi hauondolewi kwa yasiyokuwa matabano na dawa zinazokubalika katika Shari´ah. Isipokuwa mchawi ndiye anayeuondosha kwa kuwaabudia mashaytwaan. Hapana vibaya kuuondoa kwa matabano na dawa zinazokubalika katika Shari´ah. Miongoni mwa tiba bora ni zile du´aa za kinga za Kishari´ah:

أعوذ بكلمات الله التامات من شر ما خلق

“Najilinda kwa maneno ya Allaah timilifu kutokamana na shari ya alivyoviumba.”[1]

Aseme hivo asubuhi na jioni.

Asome Suurah ”al-Ikhlaasw”, ”al-Falaq” na ”an-Naas” mara kadhaa asubuhi na jioni na wakati wa kulala. Zote hizi ni miongoni mwa sababu za kujilinda.

[1] Muslim (2708).

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24605/ما-صحة-مقولة-لا-يحل-السحر-الا-الساحر
  • Imechapishwa: 12/11/2024