as-Sulamiy amesema:
“Mashaykh wengi walimraddi al-Hallaaj na kumkanusha. Walikataa asiwe na nafasi katika Taswawwuf. Ibn ´Atwaa´, Ibn Khafiyf na an-Naswraabaadhiy wakamkubali.”[1]
Tumekwishatangulia kwamba Ibn Khafiyf alijitenga mbali na maoni ya al-Hallaaj. Muhammad bin Yahyaa ar-Raaziy amesema:
“Nimemsikia ´Amr bin ´Uthmaan akimlaani al-Hallaaj na akisema: “Lau ningekuwa na uwezo juu yake basi ningemuua kwa mikono yangu.” Nikasema: “Ni kipi Shaykh alikuwa nacho dhidi yake?” Akasema: “Siku moja nilisoma Aayah kutoka ndani ya Qur-aan akasema: “Nami naweza kutunga Aayah mfano wake.”
Abu Ya´quub al-Aqtwa´ amesema:
“Nilimuoza msichana wangu kwa al-Husayn bin Mansuur [al-Hallaaj] wakati nilipoona uzuri wa njia yake na jitihada zake. Baada ya kipindi kifupi ikanibainikia kuwa ni mchawi, mtapeli na kafiri.”
Abu Ya´quub an-Nu´maaniy amesema:
“Nilimsikia Abu Bakr Muhammad bin Daawuud al-Faqiyh akisema: “Ikiwa yale aliyotemresha Allaah juu ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni haki, basi maoni ya al-Hallaaj ni batili.” Alikuwa mkali sana dhidi yake.”
[1] at-Twabaqaat (307-308).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (14/329-330)
- Imechapishwa: 17/11/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)