Swali: Vipi ikiwa mbwa atamgusa na mkono wake una unyevu?

Jibu: Udhahiri ni kama kitu kingine chochote, atauosha. Maoni sahihi ni kwamba ni najisi. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema:

“Kukitwahirisha chombo cha mmoja wenu anapokiramba mbwa anakiosha mara saba, muosho wa kwanza kwa mchanga.”

Lakini akimgusa ilihali na yeye ni mkavu haidhuru kitu.

Swali: Je, anapaswa kuosha mikono yake mara saba?

Jibu: Hili ndilo ndio dhahiri zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24702ما-يفعل-من-لمس-الكلب-ويده-رطبة
  • Imechapishwa: 29/11/2024