Mayahudi na manaswara kujenga makanisa katika miji ya waislamu

Swali: Je, inafaa kwa mayahudi na manaswara kudhihirisha makanisa yao katika nchi za waislamu?

Jibu: Hapana, wanazuiwa; isipokuwa kama nchi ilifunguliwa na tayari yalikuwepo makanisa na kisha mtawala wa waislamu akawakubalia waendelee nayo. Wanakubaliwa kubaki na makanisa yao waliyonayo.

Swali: Je, wanaruhusiwa kujenga makanisa mapya kutoka mwanzoni?

Jibu: Hapana, hawaruhusiwi kujenga makanisa mapya kutoka mwanzoni.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25417هل-لليهود-والنصارى-بناء-الكناىس-في-بلاد-الاسلام
  • Imechapishwa: 23/03/2025