Swali: Nini maana ya maneno ya Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) katika ”an-Nuuniyyah” yake:

ن ya mayahudi na ل ya Jahmiyyah
katika maneno ya Mola wa ´Arshi zimezidishwa?

Jibu: Mayahudi waliambiwa waseme:

حِطَّةٌ

“Tuondolee uzito wa dhambi!” (02:58)

badala yake wakaongeza ن na kusema:

حنطة

“Ngano.”

Wakaongeza ن ambayo Allaah hakuteremsha katika Tawraat.

Ashaa´irah na wafuasi wao wanafasiri kulingana na kuwa juu (الإستواء) kwamba maana yake ni kutawala  (الإستيلاء). Hii ni ل yao. Inatakiwa iwe اسْتَوَى na si اسْتَوَلى.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (81) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/%D8%B4%D8%B1%D8%AD%20%D9%81%D8%AA%D8%AD%20%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%AC%D9%8A%D8%AF%20-24-07-1439%20%D9%87%D9%80.lite_.mp3
  • Imechapishwa: 20/10/2018