Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuvaa vifuniko vya mikono? Ni ipi hukumu ya kuvaa nguo zinazobana mbele ya wanawake?

Jibu: Vifuniko vya mikono havina tatizo maadamu hayuko ndani ya Ihraam. Ama akiwa ndani ya Ihraam, asivae vifuniko vya mikono. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kuvaa glavu kwa aliye Muhrim katika Hajj au ´Umrah. Lakini asipokuwa katika Ihraam, hakuna tatizo kuzivaa mbele ya wanaume ili kufunika mikono yake. Hili ni jambo zuri. Vilevile anaweza kufunika mikono yake kwa mavazi mengine kama vile ´Abaa´ah, joho au mfano wake. Lakini katika Ihraam asivae vifuniko vya mikono katika Hajj au ´Umrah.

Vivyo hivyo nguo zinazobana hazijuzu, ni mamoja kwa mwanaume au mwanamke. Nguo zinazobana ambazo zinaonyesha maumbile ya sehemu za siri na kusababisha fitina hazivaliwi. Bali ziwe za wastani, ziwe na unene wa kufunika na ziwe za wastani; si pana mno na si kubana kunakoonyesha ukubwa wa sehemu za siri. Hii ni kwa wote, mwanaume na mwanamke, ingawa makatazo kwa mwanamke ni zaidi khaswa pale ambapo anaonekana na wanaume ambao ni Mahram na wasiokuwa Mahram.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/29420/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D9%84%D8%A8%D8%B3-%D8%A7%D9%84%D9%82%D9%81%D8%A7%D8%B2%D9%8A%D9%86-%D9%88%D8%A7%D9%84%D8%B6%D9%8A%D9%82%C2%A0%D9%84%D9%84%D9%85%D8%B1%D8%A7%D8%A9
  • Imechapishwa: 13/08/2025