Swali: Kuhusu mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), inapokuja siku ya tarehe 12 ya Rabiy´ al-Awwal, kijiji chote hufanya sherehe ya maulidi. Je, kuna sherehe kama hii katika Shari´ah?
Jibu: ´Ibaadah ni kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Maana yake ni kwamba muislamu hafanyi chochote miongoni mwa ´ibaadah isipokuwa kwa dalili kutoka kwa Shari´ah. Vinginevyo huwa ni miongoni mwa Bid´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakika yule atakayeishi kipindi kirefu katika nyinyi basi atakuja kuona tofauti nyingi. Hivyo basi jilazimisheni na Sunnah zangu na Sunnah za makhaliyfah wangu waongofu na wenye kuongoza baada yangu. Shikamaneni nazo barabara na ziumeni kwa magego yenu. Tahadharini na mambo ya kuzua! Hakika kila kitachozuliwa ni Bid´ah na kila Bid´ah ni upotevu.”[1]
“Hakika mazungumzo bora ni Kitabu cha Allaah, mwongozo bora ni mwongozo wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), mambo mabaya kabisa ni mambo yaliyozuliwa, kila Bid´ah ni upotofu.”
Kwa hiyo tukitafuta dalili ya maulidi kutoka ndani ya Qur-aan, katika Sunnah ya Mtume Wake, katika mwenendo wa Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na makhaliyfah wake waongofu, hata katika matendo ya karne bora tatu au nne baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), hatupati kuona kuanzishwa kwa maulidi. Kwa kuwa hakuna dalili kutoka katika Qur-aan, Sunnah, vitendo vya makhaliyfah waongofu, vitendo vya Maswahabah wala vitendo vya karne bora, hapana shaka yoyote kwamba ni Bid´ah iliyozushwa na kila Bid´ah ni upotofu.
Isitoshe kusimamisha maulidi au sherehe ya maulidi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni jambo limekatazwa kwa upande mwingine, kwa sababu ni kufananisha manaswara ambao husherehekea kuzaliwa kwa al-Masiyh ´Iysaa bin Maryam (´alayhis-Salaam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msinifu kwa kupitiliza kama walivyopindukia wakristo kwa ´Iysaa bin Maryam. Hakika mimi ni mja. Hivyo semeni “Mja wa Allaah na Mtume Wake.”[2]
Sherehe za mazazi ni sababu ya kupindukia na kuvuka mipaka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama ilivyo dhahiri. Mara nyingi maulidi yanajumuisha ushirikina na kuvuka mipaka juu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), uimbaji wa mashairi ya kishirikina ambayo ndani yake kuna kumuomba ulinzi Mtume na kumwomba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama shairi la al-Burdah na mfano wake, yenye shirki kubwa nyingi. Mfano wake ni pale aliposema:
Ee mtukufu zaidi wa viumbe! Sina mwengine zaidi yako wa kumkimbilia wakati wa majanga
Usiponitukuza siku ya Qiyaamah na ukanishika mkono, nimeangamia.
Katika ukarimu wako ni pamoja na dunia hii na mali zake
na miongoni mwa elimu zako ni pamoja na elimu ya Ubao na Kalamu
Amemfanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye kinga na kimbilio katika shida. Ulimwengu na Aakhirah ni sehemu ya ukarimu wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aidha amefanya elimu ya Ubao na Kalamu – ambayo kwayo Allaah ameandika makadirio – yote hayo wakaifanya ni sehemu ya elimu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Huku ni kuchupa mipaka na kuvuka mipaka kubaya mno. Ulimwengu na Aakhirah ni milki ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kimbilio hakitakiwi liwe kwa kiumbe, bali kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) pekee, khaswa wakati wa shida na dhiki.
Kwa hivyo kusherehekea maulidi ni miongoni mwa Bid´ah zilizozushwa tena za maovu, ambazo zimetokea baada ya kupita kwa karne bora. Ndani yake kuna kujifananisha na mayahudi na manaswara. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Yeyote mwenye kujifananisha na watu basi huyo ni katika wao.”[3]
Manaswara ndio wanaosherehekea kuzaliwa kwa al-Masiyh tangu zamani. Basi kwa nini Maswahabah hawakufanya sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Basi kwa nini waislamu hawakufanya sherehe ya kuzaliwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kama walivyofanya manaswara sherehe ya kuzaliwa kwa al-Masiyh? Iisipokuwa tu kwa sababu ya kujizuia kujifananisha nao. Hii ni dalili kwamba sherehe ya maulidi ni miongoni mwa Bid´ah ovu zilizozushwa. Isitoshe ndani yake kuna shirki kubwa au ndogo, kutumia mali katika kumuasi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), kupoteza muda na mambo mengineyo.
Kwa hivyo ni wajibu kwa waislamu wawe na tahadhari juu ya jambo hili, watosheke na yale ambayo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amewawekea katika Shari´ah, kwa kuwa ndani yake kuna kheri na baraka na furaha ulimwenguni na Aakhirah.
[1] Ahmad (16692) at-Tirmidhiy (2676).
[2] al-Bukhaariy (3445).
[3] Ahmad (5114, 5115 na 5667), al-Khatwiyb katika ”al-Faqiyh wal-Mutafaqqih” (2/73) na Ibn ´Asaakir (1/96) kupitia kwa ´Abdur-Rahmaan bin Thaabit bin Thawbaan.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/690-692)
- Imechapishwa: 09/09/2025

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/690-692)
Imechapishwa: 09/09/2025
https://firqatunnajia.com/maulidi-kujifananisha-na-mayahudi-na-wakristo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket