Matumizi ya watoto baada ya wanandoa kuachana

Swali: Mwanamke hampendi mumewe na yeye mwanaume pia ndivo anavosema. Anauliza kama kwa mujibu wa Shari´ah mume analazimika kumhudumia yeye mwanamke na watoto wake baada ya talaka akiwa katika nyumba tofauti?

Jibu: Wakiachana, basi inawapasa wapate suluhu kuhusu masuala ya watoto katika matumizi. Waangalie hali yao katika mahakama, wafanye suluhu yeye pamoja na walii wake kuhusu matumizi yanayohitajika kila mwezi. Wakigombana, basi warudi mahakamani. Mahakama itaangalia na kukadiria matumizi yanayowajibika. Lakini kilicho bora zaidi kuliko kwenda mahakamani ni suluhu. Ni bora wafanye suluhu kuhusu matumizi yanayofaa ambayo atawatumia watoto wake ikiwa amempa talaka na ana watoto. Hicho ndicho kilicho bora. Wakigombana, basi warudi mahakamani. Hakuna njia nyingine isipokuwa mahakama ndiyo inayotazama jambo hili.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1283/النفقة-على-الاولاد-بعد-طلاق-امهم
  • Imechapishwa: 15/02/2026