Matumizi kwa mke, wazazi na watoto 

Kitu kidogo ambacho mtu anamlisha mke wake analipwa thawabu kwacho akikusudia uso wa Allaah. Pamoja na kwamba mtu kuhudumia mke ni jambo la wajibu. Ikiwa humuhudumii utaambiwa ufanye hivo au mtaliki. Hata hivyo ukimhudumia mke wako kwa kukusudia uso wa Allaah, basi Allaah atakulipa ujira kwa hilo.

Kadhalika ukiwahudumia watoto wako, mama yako, baba yako, bali hata ukijihudumia wewe mwenyewe kwa kukusudia uso wa Allaah, basi Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) atakulipa thawabu kwa jambo hili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/45)
  • Imechapishwa: 23/01/2023