Kila kitu ambacho mtu anakiacha kwa ajili ya Allaah hakirejelei. Katika hayo kunaingia pia watu wengi waliyojaaliwa na Allaah kuondos TV kwenye majumba yao hali ya kutubia kwa Allaah na kujitenga nayo mbali na maovu yanayopatikana humo, watu hawa wameuliza kama kwa hivi sasa wanaweza kuirudisha nyumbani? Jibu tunawaambia hapana. Baada ya kuwa mmeshaitoa kwa ajili ya Allaah msiirudishe tena. Kwa kuwa mtu akiacha kitu kwa ajili ya Allaah na akakihama kwa ajili Yake hakirejelei.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/47)
  • Imechapishwa: 23/01/2023