Swali: Tumesikia tofauti ya maoni kuhusu mafuta ya ngamia, matumbo na utumbo wake. Baadhi ya watu wanasema kwamba navyo vinachukuliwa kuwa ni sawa na nyama yake na kwamba hakuna dalili ya kuvitoa katika hukumu hiyo. Wengine wanasema kwamba Hadiyth imetaja nyama tu na kwa ajili hiyo hakuna kutawadha kwa sababu ya kula mafuta na matumbo. Ni yepi maoni sahihi katika jambo hili? Ikiwa mtoto wa ngamia atazaliwa, kisha akachinjwa kabla hajanyonya maziwa, je, anachukuliwa kuwa ni miongoni mwa nyama au miongoni mwa matumbo na utumbo?
Jibu: Wudhuu´ hauchenguki isipokuwa kwa kula nyama, kama ilivyokuja katika Hadiyth Swahiyh ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtawadhe kwa sababu ya kula nyama ya ngamia.”
Anaingia katika hukumu hiyo pia mtoto mdogo wa ngamia, hata kama hajanywa maziwa, kutokana na kuenea kwa Hadiyth.
- Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/275-276)
- Imechapishwa: 09/11/2026
Swali: Tumesikia tofauti ya maoni kuhusu mafuta ya ngamia, matumbo na utumbo wake. Baadhi ya watu wanasema kwamba navyo vinachukuliwa kuwa ni sawa na nyama yake na kwamba hakuna dalili ya kuvitoa katika hukumu hiyo. Wengine wanasema kwamba Hadiyth imetaja nyama tu na kwa ajili hiyo hakuna kutawadha kwa sababu ya kula mafuta na matumbo. Ni yepi maoni sahihi katika jambo hili? Ikiwa mtoto wa ngamia atazaliwa, kisha akachinjwa kabla hajanyonya maziwa, je, anachukuliwa kuwa ni miongoni mwa nyama au miongoni mwa matumbo na utumbo?
Jibu: Wudhuu´ hauchenguki isipokuwa kwa kula nyama, kama ilivyokuja katika Hadiyth Swahiyh ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtawadhe kwa sababu ya kula nyama ya ngamia.”
Anaingia katika hukumu hiyo pia mtoto mdogo wa ngamia, hata kama hajanywa maziwa, kutokana na kuenea kwa Hadiyth.
Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/275-276)
Imechapishwa: 09/11/2026
https://firqatunnajia.com/matumbo-na-mafuta-ya-ngamia-vinachengua-wudhuu-kama-nyama-yake/