Atakapofika Muzdalifah, ataswali Maghrib na ´Ishaa kabla ya kushusha mizigo. Ataswali kwa   kuzikusanya. Kisha atalala hapo.

Kisha ataswali Fajr wakati wa giza la kabla ya kuchomoza kwa alfajiri. Atakuja mahali Takatifu pa kusimama, atasimama hapo na kuomba du´aa. Inapendekezwa miongoni mwa maombi yake aseme:

اللهم كما وقَفتَنا فيه، وأريتَنا إيّاه، فوفِّقنا لذكرك كما هديتنا، واغفر لنا، وارحمنا كما وعدتنا بقولك، وقولك الحق

“Ee Allaah! Umetusimamisha hapa na umetuwezesha kukiona, basi tufanikishe kukutaja kama ulivyotuongoza. Utusamehe na uturehemu kama ulivyotuahidi kwa maneno Yako – na maneno Yako ni ya kweli:

 فَإِذَا أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُوا اللَّـهَ عِندَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ ۖ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّالِّينَ ثُمَّ أَفِيضُوا مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُوا اللَّـهَ ۚ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

”Basi mtakapomiminika kutoka ‘Arafaat, mtajeni Allaah katika Mash’ar al­-Haraam na mtajeni Yeye kama alivyokuongozeni, kwani hakika kabla ya hapo mlikuwa ni miongoni mwa waliopote. Kisha miminikeni kutoka pale wamiminikapo watu na mwombeni Allaah msamaha, hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]

Atasimama mpaka mwanga uwe mkali sana, kisha ataondoka kabla ya jua kuchomoza.

[1] 2:198-199

  • Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 48
  • Imechapishwa: 09/11/2026