Matendo yanayofanywa usiku wa Qadr

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ

“Usiku wa Qadr ni mbora kuliko miezi elfu.”

Bi maana usiku wa Qadr ubora wake unalingana na miezi elfu. Matendo yanayotendeka ndani yake ni bora kuliko matendo ya miezi elfu moja tukiondoa usiku wa Qadr. Haya ni miongoni mwa mambo yanayowazindusha wale wenye busara na kuzifanya akili kuchanganyikiwa kwa vile ameuneemesha Ummah huu dhaifu nguvu juu ya nguvu kwa kuwatunuku usiku ambao matendo ndani yake ni sawa na yanashinda miezi elfu moja. Ni umri ambao mtu anaweza kuishi maisha marefu ambayo ni ya zaidi ya miaka thamanini.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taysiyr-ul-Kariym, uk. 1098
  • Imechapishwa: 16/05/2020