Swali: Ni ipi Radd kwa mwenye kusema kuwa kinachotakikana kwa mtu ni matendo na sio elimu?

Jibu: Haya ni maneno ya Suufiyyah ambao ni wapotevu. Matendo hayawezi kuwa sahihi isipokuwa yakiwa yamejengwa juu ya elimu. Matendo hayajengwi juu ya ujinga na ukhurafi wa Suufiyyah. Hizi zote ni hila za shaytwaan. Matendo hayawi [hayakubaliwi] isipokuwa mpaka yawe yamejengwa juu ya elimu sahihi. Vinginevyo matendo hayo ni batili yaliyozushwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (75) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-11-05.mp3
  • Imechapishwa: 22/08/2020