Swali: Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba watu wawili waliogombana matendo yao hayapandishwi. Wakati fulani kunatokea ugomvi kati ya watu na ugomvi huu unakuwa kwa sababu ya matusi au maapizo hayo. Hilo linapelekea yule aliyetukanwa kukasirika na anajizuia kumzungumzisha na mtu huyu anakuwa mwenye kunyimwa kwa sababu matusi au maapizo hayo. Je, ni kweli kwamba matendo yao hayanyanyuliwi kwa Allaah au hizi ni miongoni mwa Hadiyth za kuogofya?

Jibu: Hapana shaka kwamba mizozo na ugomvi kati ya watu ni sababu ya kuzuia kheri. Dalili ya hilo ni kwamba siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitoka kwa Maswahabah wake siku ya Ramadhaan ili awaeleze kuhusu usiku wenye cheo. Maswahabah wawili wakagombana ambapo elimu juu yake ikawa imenyanyuliwa katika mwaka huo.

Jengine ni kwamba matendo yanaonyeshwa kwa Allaah kila jumatatu na alkhamisi. Isipokuwa matendo ya watu wawili walio na ugomvi na kwenye mioyo yao kuna kitu katika hasira na uadui. Kuhusu hawa anasema:

“Subiri juu ya hawa wawili mpaka wapatane.”

Kwa ajili hii mtu anatakiwa kujaribu asiwe ndani ya moyo wake na kinyongo dhidi ya muislamu yeyote. Hata kama ni nafsi yenye kuamrisha sana maovu ambayo inakushawishi ufanye hivi na lile juu ya ambaye amesema au kufanya kitu fulani, ni wajibu kuondosha hilo ndani ya na moyo wao na badala yake moyo wako uwe mweupe juu ya ndugu zako waislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (36) http://binothaimeen.net/content/809
  • Imechapishwa: 15/02/2018