Matendo mema katika siku kumi za Dhul-Hijjah

Swali: Katika haya masiku kumi ya Dhul-Hijjah ni matendo yepi ambayo ni bora kufanya? Ni wajibu kwa mahujaji kufunga ile siku ya ´Arafah?

Jibu: Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna masiku yoyote ambayo matendo mema yanapendwa zaidi na Allaah kama masiku haya kumi.”

Hakuweka (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mpaka wa sampuli ya matendo mema maalum. Hivyo muislamu anatakiwa ajitahidi kufanya matendo mema kama kusema “Allaahu Akbar”. Hii ni nembo ya masiku haya. Amesema (Ta´ala):

وَاذْكُرُوا اللَّـهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ

“Mtajeni Allaah katika siku za kuhesabika.” (02:203)

Kunamaanishwa masiku kumi ya Dhul-Hijjah. Mtu anatakiwa kusema “Allaahu Akbar”, “Laa ilaaha illa Allaah” na “Subhaan Allaah” kwa wingi. Vivyo hivyo afunge masiku haya kumi ya Dhul-Hijjah. Kadhalika ajitahidi kufanya matendo mema mengine katika masiku haya. Ni masiku yenye baraka na kufanya matendo ndani kuna fadhila kubwa na thawabu nyingi. Kwa hivyo ni masiku bora na yaliyobarikiwa.

Kuhusu siku ya ´Arafah haikupendekezwa kwa mahujaji kufunga ili aweze kupata nguvu za kusimama. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisimama na huku akila na kunywa maziwa na watu wakimtazama. Alifanya hivo ili watambue kuwa hakufunga

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/15804
  • Imechapishwa: 22/08/2017