Swali: Kuna mtu amehudhuria matangamano maovu ili awakemee. Muda ulivyokuwa unaenda akaona kuwa hawezi kuwakemea, jambo likaishilia kubaki akikaa nao. Je, anapata dhambi?
Jibu: Muislamu anatakiwa kujiepusha na mikusanyiko ya maovu. Hilo ni salama zaidi juu ya dini, heshima na muruwa yake. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَاصْبِرْ نَفْسَكَ مَعَ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ وَلَا تَعْدُ عَيْنَاكَ عَنْهُمْ تُرِيدُ زِينَةَ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَا تُطِعْ مَنْ أَغْفَلْنَا قَلْبَهُ عَن ذِكْرِنَا وَاتَّبَعَ هَوَاهُ وَكَانَ أَمْرُهُ فُرُطًا
“Isubirishe nafsi yako pamoja na wale wanaomuomba Mola wao asubuhi kabla jua kucha na jioni, wanataka uso Wake, na wala macho yako yasiwavuke kwa kutaka pambo la uhai wa dunia. Na wala usimtii tuliyemghafilisha moyo wake kutokana na ukumbusho Wetu akafuata matamanio yake, na jambo lake limekuwa la kuzidi kuvuka mipaka.”[1]
وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
”Unapowaona wale wanaoziingilia na kuzishambulia Aayah Zetu, basi jitenge nao mpaka waingie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka usikae pamoja na watu madhalimu.”[2]
وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ
”Naye amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Vinginevyo mtakuwa kama wao.”[3]
Isipokuwa ikiwa mtu anaweza kuwakemea kwa mkono au mdomo wake kwa njia ya kwamba atajitenga na matangamano yao. Lakini wakipuuza makemeo yake na pengine hata wakaanza kumcheza na kumdharau, hapo analazimika kujiepusha nao. Matangamano yanamuathiri mtu. Pengine yeye mwenyewe akaanza kuyachukulia wepesi maasi. Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mioyo hukumbwa na mitihani kama vile mkeka unavyochomoka uzi mmoja baada ya mwingine. Kila pale ambapo moyo unaikubali [fitina hiyo], basi unapata doa jeusi. Na kila pale ambapo moyo unaikataa, basi unapata doa jeupe. Inazishambulia nyoyo mbili: Moyo mmoja unabaki mweupe kama jiwe tupu, haudhuriki na fitina muda wa kuwa mbingu na ardhi bado zipo, na moyo mwingine unanyonya fitina na kuwa mweusi na hafifu na kama kikombe kilichoinamishwa, ambapo hatimaye unakuwa hautambui mema na wala haukemei maovu – hakuna kingine inachokunywa isipokuwa matamanio yake.”[4]
Huenda mtu akaathirika, pengine akawa na staha kuwaambia na hivyo akaanza kupakana mafuta na kuwa pamoja nao. Kwa hivyo sawa kwake bali lazima ni yeye kuwaepuka ili wasimuathiri moyo wake, lakini ili watu wasije kufikiri kuwa matangamano hayo ni mazuri. Wanaweza kufikiri endapo ingelikuwa haramu, basi fulani na fulani wasingehudhuria.
[1] 18:28
[2] 6:68
[3] 4:140
[4] Muslim (144).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 310-311
- Imechapishwa: 06/05/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 310-311
Imechapishwa: 06/05/2025
https://firqatunnajia.com/matangamano-yanamuathiri-mtu/