Matamshi mbalimbali ya kumtakia rehema anayechemua

Swali: Zimepokelewa baadhi ya riwaya kwamba mwenye kupiga chafya aseme:

الحمد لله

”Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

na:

الحمد لله رب العالمين

”Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.”?

Jibu: Aseme:

الحمد لله

”Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

au:

الحمد لله على كل حال

”Himdi zote njema anastahiki Allaah kwa hali zote.”

au aseme tu:

الحمد لله

”Himdi zote njema anastahiki Allaah.”

au:

الحمد لله حمدًا كثيرًا

”Himdi zote njema na nyingi anastahiki Allaah.”

Zote hizi ni nzuri.

Swali: Zote zimethibiti?

Jibu: Hapana, lakini aina ya himdi imewekwa katika Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25207/ما-صيغة-الحمد-عند-العطاس
  • Imechapishwa: 22/02/2025