Maswahabah hawakuandamana

Swali:  Walinganizi wengi wabaya wanatumia hoja kujuzu kwa maandamano kwa kitendo cha Maswahabah Makkah na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akalikubali hilo. Ni yapi maoni yako kwa hilo?

Jibu: Huu ni uongo[1]. Maswahabah hawakuandamana Makkah. Hawakuharibu kitu Makkah. Walikuwa wameamrishwa kuzuia mikono yao na vurugu. Walikuwa wameamrishwa kuwa na subira mpaka walipohajiri kwenda al-Madiynah. Jihaad ikawekwa kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mambo sio ya vurugu. Huyu anawasemea uongo Maswahabah kwamba waliandamana Makkah.

[1] Tazama http://firqatunnajia.com/radd-kwa-dalili-mbili-potevu-za-kujuzisha-maandamano/

Check Also

Pale ambapo maandamano yanapelekea katika madhara makubwa zaidi

Kwanza ikiwa mtawala ni muislamu na hajatoka katika Uislamu, haijuzu kabisa kumfanya uasi. Atafanyiwa subira. …