Swali: Ipi hukumu ya kuapa kwa Talaka mara tatu? Je, Talaka inapita ikiwa kuapa kwake hakumkusudia mke na khaswa isitoshe baadhi ya watu wanafanya hivyo na hawakusudii Talaka? Na ni ipi kafara ikiwa Talaka inapita? Na je, imepita moja au mbili?
Jibu: Talaka tatu kunahitajika ufafanuzi na hatuwezi kuchukulia kwa juu juu. Ni lazima aulizwe mtu huyo aliyetamka hivyo na yajulikane makusudio yake, na matamshi aliyosema na kama hapo alitangulia kutoa Talaka au hapana. Huyu anatakiwa ahudhurie ima mahakamani kwa Qaadhiy au Daar al-Iftaah. Ama kutoa Fatwa ya jumla hapa katika Darsa Msikitini, hili sio sahihi. Kwa kuwa baadhi ya watu wanaweza kufahamu makosa na akaenda kuwaeleza watu alivyofahamu nao wakafahamu makosa. Haya ni lazima apelekewe Muftiy au Qaadhiy.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/10053
- Imechapishwa: 03/03/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related

Hakutazamwi nia ya mtamkaji talaka isipokuwa ya kinaya
https://www.youtube.com/watch?v=OcsKBXCaqV0 Swali: Ikiniteleza nikaapa kwa asiyekuwa Allaah pasina kukusudia, je mimi nitakuwa mwenye madhambi kwa hilo? Na lipi ni kubwa; kufanya hivyo au Zinaa na kunywa pombe? Jibu: Mwenye kufanya hivyo kakusudia kuapa kwa Talaka (na si kwa asiyekuwa Allaah). Mtu akiapa kwa Talaka, je Talaka inapita au inakuwa ni…
In "´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan"

Kutofautiana kwa wanachuoni katika kuapa kwa talaka
https://www.youtube.com/watch?v=APyDfwFyOq8 Swali: Ni yapi maoni yako kwa watu ambao daima wanaapa Talaka kwenye ndimi zao, kwa kusema: "Ni juu yangu Talaka nikitimiza." Na huenda akatimiza hilo na wakati mwingine huenda asitimize. Je, kwa hilo Talaka hupita? Jibu: Akinuia kupita, inapita kwa Ijmaa´. Ama akinuia yamini; kama kufanya, kuhimiza au kukataza…
In "´Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan"
Talaka ya mwenye wasiwasi inapita?
Swali: Talaka ya mtu mwenye wasiwasi inapita? Jibu: Talaka ya mtu mwenye wasiwasi aende kwa Muftiy au Qaadhiy. Masuala ya talaka ni lazima yathibitishwe na yahakikishwe. Hili linakuwa kwa kuhudhuria mtalikiwa kwa Muftiy au Qaadhiy.
In "Talaka"