Masomo ya chuo kikuu kwa shahada ya ghushi

Swali: Kuna mtu ametumia shahada ya mtu mwingine ili aweze kusoma katika chuo kikuu Saudi Arabia. Alichofanya ni kubadilisha jina kwenye shahada hii na hivyo akakubaliwa. Ni ipi hukumu ya masomo yake katika chuo kikuu hichi kwa kuzingatia ya kwamba alitafuta kwa kutumia shahada ya mtu mwingine?

Jibu: Huku ni kughushi na ni uongo. Haifai kwake kufanya hivi. Ni juu yake kuwa mkweli na asidanganye. Asiendelee kusoma kwa njia ya ghushi. Ni lazima kwake kuanza masomo mwanzo kwa shahada yake yeye mwenyewe.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-qrran-19-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020