Abu Waliyd ´Ubaadah bin Swaamit (Radhiya Allaahu ´anh) ameseema moja katika mambo ambayo walimpa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ahadi:
“… wasijivue katika utiifu wa mtawala isipokuwa ikiwa mtaona kufuru ya wazi kabisa ambayo mna dalili kwayo kutoka kwa Allaah.”
Ametaja masharti matatu ambayo tukiyaona ndio tunaweza kujivua katika utiifu wake na kujaribu kumuondosha nafasi hii. Masharti matatu:
1 – Mtaona. Ni lazima mtu awe na ujuzi. Kule kudhania tu hakujuzishi kuwafanyia uasi viongozi.
2 – Muone kufuru na si ufuska. Vovyote watavyopindukia katika maasi makubwa viongozi haijuzu kuwafanyia uasi. Ikiwa watakunywa pombe, watazini na kuwadhulumu watu haijuzu kuwafanyia uasi. Hapa ni pale ambapo tutaona kufuru ya wazi.
3 – Ya wazi. Bi maana iwe ni kufuru ilio wazi. “al-Bawaah” ni kitu kilicho wazi na dhahiri. Ama kitu ambacho kinaweza kufasiri kwa tafsiri mbali mbali haijuzu kuwafanyia uasi. Latu tukadirie watafanya kitu ambacho tunaona kuwa ni kufuru, lakini wakati huo huo pia kuna uwezekano ikawa sio kufuru, haijuzu kumfanyia uasi. Lakini ikiwa ni kufuru ya wazi, kwa mfano mtawala anawaambia wananchi kuwa pombe ni halali na kunyweni mkitakacho, liwati ni halali fanyeni liwati na mumtakaye, uzinzi ni halali fanyeni uzinifu na mnayemtaka, hii ni kufuru ya wazi na haina utata wowote. Katika hali hii ni wajibu kwa wananchi kumuondosha kwa kutumia njia yoyote hata kama itakuwa kwa njia ya kumuua. Kwa kuwa hi ni kufuru ya wazi.
4 – Ambayo mna dalili kwayo kutoka kwa Allaah. Bi maana mna dalili yenye nguvu inayoonesha kuwa kitendo hichi ni kufuru. Lau kuthibiti kwa dalili itakuwa ni dhaifu au katika kustadili kwake kuna udhaifu, katika hali hii haijuzu kumfanyia uasi. Kwa sababu kufanya uasi kuna shari na madhara makubwa.
Endapo tutaona mambo haya haijuzu kumuondosha mpaka tuwe na uwezo wa kufanya hivo. Ikiwa hatuna uwezo haijuzu kumuondosha. Kwa sababu pengine tukijaribu kumuondosha na siis hatuna uwezo akajilipiza kwa watu wema wengine. Masharti haya yanajuzisha au kuwajibisha kujivua katika utawala wa kiongozi, lakini hata hivyo kwa sharti tuwe na uwezo. Ikiwa hatuna uwezo haijuzu kufanya hivo kwa sababu kitendo hichi ni mtu kuitia nafsi yake mwenyewe katika maangamivu. Kuna faida gani lau tutafanya uasi kwa mtawala huyu ambaye tumeona kwake kufuru ya wazi kabisa na sisi hatupambani naye isipokuwa kwa kutumia [nguvu ya] visu vya kupikia na yeye ana silaha nzito nzito? Hakuna faida yoyote. Maana ya hili ni kuwa tumetoka ili kuziangamiza nafsi zetu.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/422-423)
- Imechapishwa: 11/08/2025

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/422-423)
Imechapishwa: 11/08/2025
https://firqatunnajia.com/masharti-ya-kujivua-katika-utiifu-wa-mtawala/