Mashaka juu ya nyama zinazouzwa katika maduka ya makafiri zilizoandikwa ”حلال”

Swali:  Kuhusiana na sisi wanafunzi ambao tunaishi nje katika miji ya makafiri tuna swali kuhusu nyama; hatujui jinsi gani wanavyochinja japokuwa wanaandika kwenye pakiti neno ”حلال” lakini bado tukawa na mashaka yanayotokamana na maneno ya watu juu ya nyama hizo. Je, tule au tusile[1] ?

Jibu: Yeye hajui kuwa wale waislamu wachache wanaoshi katika miji ya makafiri na mkusanyiko wa wanafunzi hivi sasa wamewatengenezea vichinjwa ambapo wanaweza kupata nyama. Tatizo lao limekwisha na himdi zote anastahiki Allaah. Wakiwa na uwezo wa kununua nyama zinazouzwa na waislamu walizochinja basi wafanye hivo. Vinginevyo wale samaki. Samaki huhitaji kuwa na shaka. Kula samaki. Jiepushe na nyama zilizo na mashaka. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Jiepushe na lenye kukutia mashaka na liendee lisilokuwa na mashaka.”

“Atakayejiepusha na mambo ya utata basi ameitakasa dini na heshima yake.”

Jiepushe na mambo haya. Nyama yenye kusifiwa ni samaki zilizoenea huko.

[1] Tazama Sio lazima ule nyama katika nchi za makafiri – al-Firqah an-Naajiyah (firqatunnajia.com)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/ar/node/2611
  • Imechapishwa: 17/01/2018