Masanamu yanayofaa na yasiyofaa kutengenezwa

Swali: Ni ipi hukumu ya kutengeneza sanamu?

Jibu: Kutengeneza masanamu yenye maumbile ya viumbe wenye roho, ni haramu na haijuzu. Kwa sababu imethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani watengeneza picha. Imethibiti pia kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Ta´ala) amesema: “Ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule ambaye anajaribu kuumba mfano wa viumbe Wangu? Hebu waumbe mdudu chungu, waumbe punje ya nafaka au waumbe chembe ya shayiri.”[1]

Kwa hiyo ni haramu. Lakini masanamu hayo sio ya maumbile ya viumbe wenye roho hapana vibaya na ni halali kula mapato yake kwa sababu yanatokana na kazi ambayo ni halali.

[1] al-Bukhaariy (5953) na (7559) na Muslim (2111).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/320)
  • Imechapishwa: 28/02/2026