Swali: Upande mmoja Allaah (´Azza wa Jall) anaeleza kuwa Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

مَا هَـٰذِهِ التَّمَاثِيلُ الَّتِي أَنتُمْ لَهَا عَاكِفُونَ

”Nini haya masanamu ambayo nyinyi mnayakalia kuyaabudu?”[1]

Upande mwingine Allaah (´Azza wa Jall) amesema kuhusu maaskari wa Sulaymaan (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

يَعْمَلُونَ لَهُ مَا يَشَاءُ مِن مَّحَارِيبَ وَتَمَاثِيلَ وَجِفَانٍ كَالْجَوَابِ وَقُدُورٍ رَّاسِيَاتٍ ۚ اعْمَلُوا آلَ دَاوُودَ شُكْرًا ۚ وَقَلِيلٌ مِّنْ عِبَادِيَ الشَّكُورُ

”Wanamfanyia kazi atakayo kujenga ngome ndefu za fakhari na masanamu na madeste makubwa kama mahodhi na masufuria makubwa yaliyothibiti imara. Fanyeni kazi, enyi familia ya Daawuud, kwa kushukuru – na wachache miongoni mwa waja Wangu ni wenye kushukuru!”[2]

Ni vipi tutaoanisha masanamu yaliyoharamishwa katika Aayah ya kwanza na katika Aayah ya pili ambapo wamezingatiwa kuwa ni neema alopewa?

Jibu: Masanamu yaliyotajwa katika Aayah kuhusu Ibraahiym (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kulikusudiwa kwa sababu yalikuwa yakiabudiwa. Masanamu yaliyotajwa kuhusu Sulaymaan  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kulikusudiwa kwa sababu ya pambo. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

لِكُلٍّ جَعَلْنَا مِنكُمْ شِرْعَةً وَمِنْهَاجًا

“Kwa kila Ummah katika nyinyi Tumeujaalia Shari’ah na mfumo wake.”[3]

Yalikuwa yenye kuruhusiwa kwa Sulaymaan ambapo Shari´ah yetu ikaja kuyakataza. Mosi ni kwa sababu ya kuigiliza uumbaji wa Allaah, pili ni kwa sababu yanaabudiwa.

[1] 21:52

[2] 34:13

[3] 05:48

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 349-350
  • Imechapishwa: 07/07/2025