Maradhi na matatizo mbalimbali ni sababu ya kufutiwa madhambi

Swali: Mtu akifanya maovu na akapatwa na maradhi kwa sababu ya maovu haya – je, ni majaribio kutoka kwa Allaah?

Jibu: Mtu akifanya dhambi na akapatwa na maradhi, basi maradhi haya yanamfutia dhambi zake. Bali mtu akidungwa na mwiba basi Allaah anamfutia makosa yake kwao. Bali mtu akihisi hamu na dhiki, Allaah anamfutia makosa yake. Hayo yamepokelewa katika Hadiyth ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema waziwazi. Hii ni neema ya Allaah (´Azza wa Jall) kuwa mtu akipatwa na maradhi au akahisi hamu kwamba inakuwa ni kafara ya makosa yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1471
  • Imechapishwa: 16/01/2020