Swali: Katika baadhi ya nyakati mja anatamani kifo na kukutana na Mola wake (Jalla wa ´Alaa) na mara nyingine anayachukia mauti.
Jibu: Hayo ni katika maumbile kwamba wanachukia kifo. Hayo ni kutokana na maumbile ya watu. Ni kama alivosema ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) baada ya Mtume kusema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Yule mwenye kupenda kukutana na Allaah, basi Allaah atapenda kukutana naye. Na yule mwenye kuchukia kukutana na Allaah, basi Allaah atachukia kukutana naye.” Ndipo ´Aaishah akasema: ”Ee Mtume wa Allaah! Je, unakusudia kifo? Sote tunachukia kifo.”
Kwa hivyo maumbile yanayoshika nafasi kubwa kwa mtu ni kwamba anachukia kifo na anapenda kuishi. Muumini anapenda kuzidisha matendo mema, na asiyekuwa muumini anapenda kuendelea kustarehe na matamanio yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamjibu:
”Hapana, lakini muumini anapofikiwa na mauti na akapewa bishara njema za Pepo basi hapo hupenda kukutana na Allaah na Allaah naye akapenda kukutana naye. Kafiri anapofikiwa na kifo na akapewa bishara mbaya za Moto basi hapo huchukia kukutana na Allaah na Allaah naye akachukia kukutana naye.”
Au alisema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) maneno yanayofanana na hayo.
Baadhi ya nyakati mtu anaingiwa moyoni mwake na shauku ya kifo ili aweze kukutana na Mola wake kwa sababu anamdhania vyema Allaah, anatamani kukutana Naye, kutamani yale yaliyoko Kwake na kutokana na yale maovu, mabalaa, maharibifu na khatari anayoyaona ulimwenguni, tamaa kama hiyo inaweza kumtokea muumini. Hata hivyo licha ya haya yote haijuzu kwake kuomba kifo au hata kukitamani, kama ilivyokuja katika Hadiyth ambazo ni Swahiyh ambazo zinakataza kufanya hivo. Hiyo ni rehema ya Allaah Kwake na ile furaha, raha na starehe ambayo Allaah anamuharakishia.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24479/حكم-كراهية-المومن-للموت
- Imechapishwa: 04/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)