Mara akiswali na Sutrah, mara bila Sutrah

Swali: Je, kuweka Sutrah ni wajibu?

Jibu: Dhahiri ya Hadiyth inaonesha kuwa ni wajibu, kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Anaposwali mmoja wenu, basi aswali kuelekea kwenye Sutrah na aikaribie.”

Hata hivyo kinachotambulika kwa wanazuoni ni kwamba ni Sunnah iliyosisitizwa, kwa sababu imepokelewa kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba aliswali katika baadhi ya sehemu bila Sutrah, kama alivyopokea al-Fadhwl bin al-‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhumaa). Kitendo chake cha yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuswali bila Sutrah wakati mwingine kunajulisha ya kwamba si wajibu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28937/هل-السترة-للمصلي-مستحبة-ام-واجبة
  • Imechapishwa: 13/05/2025