Mapenzi baina ya wanandoa ni ya kimaumbile na sio ya kidini

Swali: Mapenzi ya mume kumpenda mke wake na kumwambia “Mimi siwezi kuishi bila ya wewe”, je, haya ni mapenzi ya kumpenda asiyekuwa Allaah na kujifungamanisha na asiyekuwa Yeye?

Jibu: Haya ni mapenzi ya kimaumbile:

وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً

“Amekujaalieni baina yenu mapenzi na rehema.” (30:21)

Haya ni mapenzi ya kimaumbile na sio mapenzi ya ´Ibaadah. Hakuna neno kwayo.

Check Also

Peleka mahakamani

Swali: Mimi nina dada anayegombana na mume wake mwenye madhehebu na mfumo wa Suufiyyah. Anampiga, …